Afrika yaona ukuaji endelevu wa mifumo ya malipo ya papo hapo
2023-11-10 08:14:32| CRI

Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA), imesema Afrika inashuhudia ukuaji endelevu na mahitaji ya mifumo ya malipo ya papo hapo na mahitaji.

Toleo la pili ya ripoti ya kila mwaka ya mfumo jumuishi wa malipo ya papo hapo (SIIPS) barani Afrika, inasema mafanikio hayo yanaonyesha maendeleo madhubuti ya Afrika kuelekea lengo linalotarajiwa la kuwa na mifumo ya malipo ya papo hapo ya kina na shirikishi, kama sehemu ya Miundombinu ya Kidijitali ya Umma ya Afrika (DPI), inayounda mfumo ikolojia wa kidijitali kwa watu, biashara na serikali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mifumo mitatu mipya ya malipo ya papo hapo ambayo imezinduliwa nchini Ethiopia, Morocco na Afrika Kusini katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, na kufanya jumla ya mifumo ya papo hapo ya ndani ya nchi na ya kikanda katika bara la Afrika kufikia 32.

Ripoti pia imesema mifumo hiyo imewezesha karibu miamala bilioni 32 yenye thamani ya takriban dola trilioni 1.2 za Marekani kwa mwaka 2022.