Rais Xi ajibu barua kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Philadelphia Orchestra
2023-11-10 20:16:54| cri

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua kutoka kwa Matias Tarnopolsky, Mkurugenzi Mtendaji wa Orchestra ya Philadelphia.

Kwenye majibu yake  Rais Xi amesema amefurahishwa kujua kwamba Orchestra ya Philadelphia itafanya ziara nchini China mwezi Novemba kwa mara ya 13 na kushirikiana na Wachina kuandaa shughuli mbalimbali za maonyesho, kuadhimisha ziara yake ya kwanza nchini China mnamo 1973 na kuendelea na muziki na urafiki na watu wa China kwa nusu karne.

Miaka 50 iliyopita, orchestra ya Philadephia ilianza safari ya  mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Marekani, ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kurudisha uhusiano kati ya China na Marekani. Rais Xi amesema katika miaka 50 iliyopita, orchestra hiyo imefanya ziara China mara 12, ikiwa kama "balozi wa  utamaduni" anayefanya kazi ya hamasa kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani.