Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri kutoka nchi 22 za Afrika kujadili mambo ya fedha na jinsia
2023-11-14 13:53:54| cri

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wanaohusika na fedha na masuala ya jinsia utakaofanyika kuanzia Novemba 15 hadi 17.

Mkutano huu ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mambo ya Wanawake na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF Afritac East) utawakutanisha mawaziri kutoka nchi 22 barani Afrika. 

Waziri wa fedha wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema mkutano huo utatoa fursa kwa washiriki kujadili namna bora ya kushughulikia athari za mapungufu ya kijinsia katika uchumi jumla.