Watu watano wafariki kutokana na mafuriko kaskazini mwa Tanzania
2023-11-14 08:52:18| CRI

Watu watano wamefariki kutokana na mafuriko ya ghafla yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha mfululizo katika wilaya ya Arusha, kaskazini mwa Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amesema mamlaka wilayani humo zinafanya tathmini kujua uharibifu uliotokana na mafuriko hayo. Amesema mpaka sasa watu watano wamefariki kutokana na mafuriko hayo, lakini hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa kuwa nyumba nyingi katika mteremko wa Mlima Meru zimezama katika maji.

Bw. Mtahengerwa ametaka wakazi katika maeneo yaliyoathirika kuwa watulivu kwa kuwa mamlaka zinajitahidi kukarabati miundombinu iliyoharibika na kuhamisha watu ambao nyumba zao zimeharibika kutokana na mafuriko hayo.