Rais Xijinping atuma barua ya pongezi kwa mkutano wa mwaka wa 10 wa wanaviwanda wa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan
2023-11-14 13:55:56| cri

Rais Xijinping ametuma barua ya pongezi kwa mkutano wa mwaka wa 10 wa wanaviwanda wa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan, akisema: "Wakati inapofika mwaka wa 10 wa tangu kuanzishwa kwa mkutano kati ya wanaviwanda wa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan, natoa pongezi wa kidhati kwa wajumbe wote wa mkutano huo! Uchumi wa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan wote ni uchumi wa kabila la Wachina, ndugu wa pande zote mbili wana mustakabali wa pamoja. Mkutano huo ni jukwaa muhimu la mawasiliano na ushirikiano kati ya wanaviwanda na wafanyabiashara wa pande zote mbili, na umetoa mchango mkubwa kwa kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya pamoja kati ya pande mbili. Anatarajia kuwa mkutano huo utashirikisha wanaviwanda na wafanyabiashara kati ya pande mbili, kustawisha uchumi wa kabila la Wachina, kuhimiza maslahi za ndugu za pande mbili, na kutoa mchango mpya kwa muungano wa China."