Jeshi la Sudan na kikosi cha RSF vyagombea kambi ya jeshi la anga kusini mwa Khartoum
2023-11-14 08:49:25| CRI

Mapigano makali yameendelea kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) ili kudhibiti kambi ya jeshi la anga kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Mapigano hayo yalilenga Kambi ya Jeshi la Anga ya Al-Nujoumi katika eneo la Jabal Awliya, kilomita 50 kusini mwa Khartoum, karibu na Jimbo la White Nile.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mafunzo ya Al-Gitaina katika Jimbo la White Nile, Reem Ahmed amesema katika taarifa yake kwamba, hospitali hiyo imepokea watu 18 waliojeruhiwa kutoka Jabal Awliya kutokana na mapigano mapya katika eneo hilo yaliyosababisha vifo vya watu watatu na wengine 15 kujeruhiwa, ambao wote ni askari wa Jeshi la Sudan.

Jeshi hilo limepinga madai ya RSF kwamba limeteka Kambi ya Jeshi la Anga ya Al-Nujoumi, na kusema kambi hiyo bado iko chini ya udhibiti wake.