Wapalestina 31 wauawa katika shambulio la Israel dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Jabalia
2023-11-14 08:50:22| CRI

Vyanzo vya usalama na wahudumu wa afya nchini Palestina vimesema watu 31 wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio la Israel lililolenga makazi kadhaa katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Idara ya Ulinzi wa Raia iliyo chini ya kundi la Hamas imesema katika taarifa yake kuwa, ndege ya kijeshi ya Israel ililenga eneo la makazi ya watu katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, ambapo nyumba 12 ziliharibiwa.

Ofisi ya huduma za afya ya Ukanda wa Gaza imesema, idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulio ya Israel imeongezeka na kufikia 11,240, huku wengine zaidi ya 28,000 wamejeruhiwa.