Waziri mkuu wa Ethiopia asema nchi hiyo kujiunga na BRICS kutahimiza ushirikiano wa Kusini na Kusini
2023-11-15 09:32:14| CRI

Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed Jumanne amesema nchi hiyo kujiunga na mfumo wa BRICS kutaleta faida, kwa kuwa kundi hilo linahimiza mfumo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Akijibu maswali ya wabunge katika Baraza la Chini la Bunge la Ethiopia, Bw. Abiy amesema, mambo ya kidiplomasia na mtazamo wa sera ya nje ya Ethiopia viko chini ya msingi wa kunufaishana, kuheshimu maslahi na mamlaka ya nchi, pia kuhakikisha maslahi ya uchumi wa kijamii, jiografia na historia.

Ameongeza kuwa, kujiunga na mfumo wa BRICS kunatokana na hali halisi ambayo kundi hilo linahimiza ushirikiano wa Kusini na Kusini. Amesema kwa kuwa Ethiopia ni nchi muhimu kwenye mfumo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini, kujiunga kwake na BRICS kutakuwa msukumo muhimu kwa Ethiopia na nchi wanachama wengine wa BRICS.