Uganda yaahidi kutumia mikutano ya NAM, G77+China kuimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini
2023-11-15 09:26:49| CRI

Uganda imesema itatumia mkutano wa 19 wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) na Kundi la Nchi 77 na China kuboresha ushirikiano na mshikamano wa Kusini na Kusini kati ya nchi wanachama.

Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda John Mulimba amesema jana kuwa, mikutano hiyo miwili itatoa fursa adimu kwa Uganda kuwa kituo cha masuala ya kimataifa na pia kuunga mkono na kuboresha maslahi ya nchi zinazoendelea.

Amesema kaulimbiu ya mkutano wa NAM ni “Kuimarisha Ushirikiano kwa Maslahi ya Pamoja,” huku kaulimbiu ya mkutano wa G77+China itakuwa ni “Kutomwacha Yoyote Nyuma,” ambazo msingi wake ni ukweli kwamba baadhi ya masuala yaliyojitokeza kimataifa yanahitaji ushiriki wa nchi wanachama wa makundi hayo.