Serikali ya Rwanda yafuta mikataba 13 ya uchimbaji madini kutoka na sababu za usalama na mazingira
2023-11-15 10:30:40| cri

Bodi ya Migodi, Petroli na Gesi ya Rwanda (RMB) imetangaza kufuta au kutorefusha muda wa leseni za mikataba 13 ya uchimbaji madini kutokana na "dosari zinazoendelea" zinazohusiana na kuheshimu viwango vya usalama, mazingira, na kazi na kutimiza ahadi za uwekezaji.

Uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia matokeo ya ukaguzi na ushirikiano kati ya bodi hiyo na wamiliki wa makubaliano kuhusu majukumu yao ya kisheria na kimkataba.

Makampuni mengine kadhaa yenye dosari za usalama yamepewa notisi, na yametakiwa kuwasilisha maelezo ya kuridhisha kuhusu kurekebisha dosari zilizopo

Bodi hiyo pia imesema itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ili kuhakikisha kwamba makubaliano yaliyopo yanalindwa na kutekelezwa ipasavyo huku uwekezaji mpya ukisubiriwa.