Tanzania sasa inaweza kufadhili asilimia 70% ya bajeti yake
2023-11-15 09:06:01| cri

Tanzania sasa inaweza kufadhili asilimia 70% ya bajeti yake baada ya kuanza kutekeleza mageuzi ya kiuchumi yakiwa ni pamoja na kubadilishwa kwa mbinu za ukusanyaji ushuru. Naibu rais wa Tanzania Philip Mpango amesema uwazi katika ukusanyaji kodi, raia kulipa kodi na matumizi bora ya ushuru unaokusanywa ni baadhi ya sababu ambazo zimeifanya Tanzania kupiga hatua hiyo muhimu.

 Kadhalika Dkt. Mpango amesema mamlaka za ukusanyaji ushuru nchini humo zinaendeleza mikakati ya kuwaelimisha raia kuhusu umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kutumia njia za kisasa na rahisi kukusanya ushuru. Ikumbukwe kuwa nchini nyingi za Afrika hutegemea mikipo ya nje kufadhili bajeti zao kutokana na ukusunyaji mdogo wa ushuru wa ndani, pesa ambazo zinapaswa kutumika kuendesha shughuli za taifa kama vile kulipa wafanyikazi wa umma mishahara.