Rais wa DRC azindua kituo cha kuzalisha umeme kilichojengwa na China
2023-11-15 09:36:45| CRI

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi jana amezindua kituo cha kuzalisha umeme cha Kinsuka katika kitongoji cha mji wa Kinshasa kilichojengwa na China.

Kwenye uzinduzi huo, rais Tshisekedi amepongeza kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Kinsuka, na kusisitiza kuwa, nchi yake inatamani sana kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana na China.

Kituo hicho kinatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa umeme kwa wakazi milioni 2, kupanua ukubwa wa gridi ya taifa ya DRC na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo.