Kampuni ya Base Titanium yalipa Kenya dola milioni $49.3
2023-11-15 05:03:11| cri

Kampuni ya Base Titanium, inayochimba madini ya titani katika Kaunti ya Kwale, imelipa serikali ya Kenya dola milioni $49.3 kama mirahaba na kodi kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwa mjibu wa stakabadhi za kampuni hiyo. 

Kiasi hicho cha fedha hata hivyo ni cha chini ikilinganishwa na dola milioni 51.1 ambazo Kenya ilipokea kutokana na uchimbaji madini ya Titanium mwaka wa 2022. kupungua kwa kiasi hicho cha fedha kwa asilimia 3.4% kunatokana na kupungua kwa madini katika migodi pamoja na kubadilika kwa bei ya madini kwenye soko la kimataifa.

Licha ya uzalishaji mdogo wa madini mwaka, mauzo ya madini ya Kampuni ya Base Titanium yalipungua kwa asilimia 3%  huku Kaunti ya Kwale ambapo madini hayo huchimbwa ikipokea dola milioni 22.19 kutoka dola milioni 19.6 mwaka wa 2022.