Nchi za Kusni na Mashariki ya Afrika zakabiliwa na mgogoro mkubwa wa maji na usafi
2023-11-15 09:30:35| CRI

Benki ya Dunia imesema kuwa kanda ya kusini na mashariki mwa Afrika inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa maji na usafi, ambapo asilimia 95 ya Waafrika milioni 247 ambao hawana uwezo wa kupata maji safi wakiishi katika eneo hilo.

Akizungumza katika Mkutano wa Uongozi wa Maji Safi na Usafi, kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika unaoendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia, Makamu wa rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Victoria Kwakwa amesema, kuna watu milioni 37 ambao hawana uwezo wa kupata maji, na watu wengine milioni 247 hawana huduma bora za usafi katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara ikilinganishwa na mwaka 2000.

Amesema katika kanda hiyo, kwa Zaidi ya miaka 20, upatikanaji wa kimsingi wa maji na usafi haujaendana na ongezeko la idadi ya watu, na kuongeza kuwa, bila ya upatikanaji Zaidi wa maji na huduma za usafi, eneo la Afrika mashariki na kusini litashindwa kutimiza ahadi ya kuondokana na umasikini na ustawi wa pamoja.