Kufinywa kwa bajeti ya wizara ya maji na Mazingira Uganda kumeathiri utoaji huduma
2023-11-15 22:34:42| cri

Katibu wa kudumu katika wizara ya maji na mazingira nchini Uganda Alfred Okidi Okot amesema hatua ya serikali ya nchi hiyo kupunguza mgao wa bajeti kwa wizara hiyo unalemaza maendeleo ya jamii.

Kulingana na bwana Okot, japo pesa ambazo hutengewe wizara hiyo ni za chini bado hazina ya kitaifa haizitumi kwa wizara hiyo jambo ambalo limeathiri usambazaji wa bidhaa hiyo muhimu. Katika bajeti ya mwaka mwaka huu kiasi cha fedha zilizotengewa wizara ya maji na mazingira ilipunguzwa kwa asilimia 2.2% hadi shilingi trilioni 1.6 za Uganda ikiwa ni asilimia 21% tu ya pesa zinazohitajika kuendesha shughuli za wizara hiyo.