Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kutoa dola milioni 837 kwa Morrocco
2023-11-15 03:04:51| cri

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kutoa dola milioni 837 kwa ajili ya miradi mbalimbali nchini Morocco ili kuisaidia nchi hiyo kujikwamua kutokana na uharibifu wa tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Septemba mwaka huu na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali pamoja na vifo vya zaidi ya watu 3,000. 

Akizungumza wakati wa mkutano wa uwekezaji barani Afrika unaoendelea jijini Marrakech  Morocco, rais wa AfDB Dkt Akinwumi Adesina amesema AfDB itasimama na Morocco kutokana na ujasiri wa nchi hiyo kuandaa makongamano makubwa ya kibiashara licha ya kupitia kipindi kigumu. Ikumbukwe kuwa mwezi Septemba nchi hiyo ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa benki ya dunia na shirika la fedha duniani IMF, miaka 50 baada ya mkutano huo kuandaliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika.