Maparachichi ya Kenya yapata soko lililo tayari la China baada ya kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika CIIE
2023-11-16 09:45:40| CRI

Hujambo msikilizaji na karibu sana kwenye kipindi cha Daraja kinachokujia kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Kipindi cha leo msikilizaji, mbali na habari mbalimbali kuhusu China nan chi za Afrika, pia tutakuwa na ripoti inayohusu mauzo ya Parachichi za Kenya nchini China, na pia tutakuwa na mahojioano kuhusu jinsi nchi zilizojiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China zinavyofaidika na Pendekezo hilo.