Baraza la Usalama la UM laongeza muda wa mamlaka ya ATMIS
2023-11-16 09:55:35| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano lilipitia azimio la kuongeza mamlaka ya Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kwa muda wa miezi sita hadi tarehe 30 Juni mwaka 2024.

Azimio namba 2710 lililoungwa mkono na nchi wanachama 15 wa Baraza la Usalama la UM linaidhinisha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, kutuma askari wasiozidi 17,626 kwa ATMIS kabla ya tarehe 31 Desemba mwaka 2023, na kumaliza awamu ya pili ya kupunguza wafanyakazi elfu tatu kabla ya tarehe hiyo, ambapo itakuwa wamesitisha kwa muda miezi mitatu kwa mujibu wa matakwa ya serikali ya Somalia.

Azimio hilo pia linawapa idhini askari 14,626 kuanzia tarehe mosi Januari hadi tarehe 30 Juni mwaka 2024, na kumaliza awamu ya tatu ya kupunguza wafanyakazi elfu nne wa ATMIS siku za baadaye.