Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba ya maandishi yenye kichwa cha "Kabili changamoto kwa Pamoja ili kuandika Ukurasa Mpya katika Ushirikiano wa Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa Wakuu wa Viwanda na Biashara wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) uliofanyika San Francisco, Marekani.
Rais Xi ametoa wito wa kuzingatia malengo na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kudumisha njia ya mawasiliano kati ya nchi na nchi inayoangalia mazungumzo badala ya makabiliano, ushirikiano badala ya mafungamano, na kudumisha ustawi na utulivu katika ukanda wa Asia na Pasifiki. Amesisitiza kuwa ukanda huo hauwezi na haupaswi kuwa uwanja wa vita vya siasa za kijiografia, achilia mbali kushiriki katika "vita vipya baridi" au makabiliano ya makundi. Ni lazima kuzingatia uwazi wa kikanda, kuendeleza bila kuyumba mchakato wa Eneo la Biashara Huria la Asia na Pasifiki, kukuza mwingiliano wa kiuchumi wa nchi mbalimbali, na kujenga uchumi wazi wa Asia na Pasifiki kwa ushirikiano wa kunufaishana.
Xi Jinping ameongeza kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, uchumi wa China umeendelea kuimarika, ikiwa chachu kubwa zaidi ya ukuaji wa dunia, China inakaribisha wadau wa viwanda na baishara wa nchi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kujiendeleza kisasa wa China na kunufaika na fursa kubwa zinazotokana na maendeleo ya ubora wa juu ya China.