Rais wa China akutana na Waziri Mkuu wa Japan
2023-11-17 11:06:07| cri

Rais Xi Jinping wa China jana alasiri alikutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida huko San Francisco nchini Marekani.

Rais Xi amesema, huu ni mwaka wa 45 tangu Mkataba wa Amani na Urafiki kati ya China na Japan uliposainiwa, na mkataba huo umekuwa mnara muhimu katika historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Katika miaka 45 iliyopita, uhusiano kati ya China na Japan kwa ujumla umedumisha mwelekeo wa maendeleo, umeleta manufaa kwa watu wa nchi hizo mbili na pia kutoa mchango chanya katika kuhimiza amani, maendeleo na ustawi wa kikanda.

Rais Xi amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kufuata mwelekeo wa kihistoria, kuzingatia maslahi ya pamoja, na kushughulikia tofauti zao kwa njia mwafaka. Pia pande hizo mbili zinatakiwa kushikilia kanuni zote zilizothibitishwa kwenye nyaraka nne za kisiasa kati ya China na Japan, kutambua upya hadhi ya uhusiano wa kimkakati wa kunufaishana na kuupa maudhui mapya, ili kujitahidi kujenga uhusiano wa nchi mbili unaoendana na mahitaji ya zama mpya.