Serikali ya Tanzania yaitaka MUHAS kuwa na mikakati kwa wanafunzi wa elimu ya juu ya tiba
2023-11-17 10:23:44| CRI


 

Serikali ya Tanzania imekitaka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kusimamia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi Ndaki ya Tiba (HEET) utakaojenga Kampasi ya Mloganzila na Kigoma Ujiji, ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa asilimia 30.

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Profesa Peter Msofe amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la miaka 60 ya MUHAS. Amesema uanzishwaji wa ndaki hiyo unaendana na maono ya chuo ya kufanya mageuzi na kuwa mji wa taaluma za afya kufikia mwaka 2050.

Akizungumzia kuhusu tafiti, Prof. Mkenda amesema, chuo hicho kinaongoza kwa tafiti nyingi za afya nchini humo ambazo zimeleta mapinduzi kwenye sera na miongozo inayotumika ndani na nje ya nchi hususan katika kuboresha huduma za afya, kutoa matibabu sahihi na kuzuia magonjwa.