Walimu na wanafunzi 132 wa Tanzania wapewa tuzo ya balozi wa China
2023-11-17 10:03:36| CRI

Walimu na wanafunzi 132 wa Tanzania wametangazwa washindi wa Tuzo ya Sita ya Balozi wa China kwa kutoa mchango maalumu katika kufunza lugha ya Kichina au kuwa mahodari wa kujifunza lugha ya Kichina katika mwaka 2023.

Kwenye hafla ya kutoa tuzo iliyofanyika katika ubalozi wa China nchini Tanzania, wanafunzi 125 na walimu saba wa Tanzania kutoka sekondari 18 na vyuo vikuu vitano walipewa zawadi mbalimbali.

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian alisema tangu Tuzo ya Bolazi wa China ilipoanzishwa mwaka 2018, wanafunzi wengi zaidi wa Tanzania wamejifunza lugha ya Kichina, na shule nyingi zaidi za Tanzania zimeanzisha masomo mbalimbali ya Kichina. Kwa sasa, somo la lugha ya Kichina limewekwa kwenye mfumo wa elimu wa Tanzania, hali ambayo inaonyesha uungaji mkono wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa somo la lugha ya Kichina.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda alisema kusoma lugha ya Kichina sio tu kutasaidia maendeleo ya wanafunzi, bali pia kutatoa mchango katika urafiki na ushirikiano kati ya China na Tanzania.