Rais wa China akutana na kiongozi wa Brunei
2023-11-17 10:58:02| cri

Rais Xi Jinping wa China jana huko San Francisco nchini Marekani amekutana na Sultani wa Brunei Haji Hassanal Bolkiah.

Rais Xi amesema China na Brunei zimedumisha urafiki wa jadi kwa muda mrefu, ni majirani wema wanaotengwa na bahari, na pia ni wenzi wazuri wa kuaminiana na kuungana mkono.

Amesema China inapenda kushirikiana na Brunei kuhimiza uhusiano wao kupata maendeleo mapya, na kusukuma mbele ushirikiano katika kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kuwaletea wananchi wa nchi hizo mbili manufaa zaidi.