Rais Xi ataka juhudi zote za uokoaji zifanywe baada ya ajali ya moto kutokea kwenye jengo la kampuni ya makaa ya mawe
2023-11-17 10:06:23| CRI

Rais Xi Jinping wa China ameagiza kufanywa juhudi zote za kuokoa na kuwatibu majeruhi baada ya ajali ya moto kutokea Alhamisi asubuhi kwenye jengo la kampuni ya makaa ya mawe kaskazini mwa mkoa wa Shanxi nchini China.

Xi ametaka mikoa na idara zote zinazohusika kutambua kwa kina hatari katika sekta muhimu ili kulinda maisha ya watu, mali na utulivu wa jamii.

Xi ambaye yuko ziarani nchini Marekani alitoa maagizo hayo mara baada ya ajali hiyo kutokea.

Moto huo uliotokea katika mji wa Lyuliang umesababisha vifo vya watu 26 na wengine 38 kujeruhiwa.