Rais wa China akutana na Waziri Mkuu wa Fiji
2023-11-17 11:12:51| cri

Rais Xi Jinping wa China jana huko San Francisco nchini Marekani amekutana na Waziri Mkuu wa Fiji Sitiveni Rabuka.

Rais Xi amesema China inaichukulia Fiji kuwa rafiki mzuri na mshirika mzuri, na inaunga mkono Fiji katika kuchagua njia yake ya kujiendeleza ili kutimiza ustawi wa taifa. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Fiji kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano halisi, kuimarisha mawasiliano kati ya watu na utamaduni, na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo zaidi.

Aidha Rais Xi amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na Fiji katika kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kutekeleza Pendekezo la Maendeleo Duniani, na kuisaidia Fiji kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii.