Mazungumzo ya mawasiliano ya watu kati ya China na Marekani yafanyika huko San Francisco
2023-11-17 15:56:17| cri

Mazungumzo ya mawasiliano ya watu kati ya China na Marekani yaliyoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Shirikisho la Mawasiliano ya Wanafunzi Vijana wa Marekani na China yamefanyika huko San Francisco, nchini Marekani.

Mkuu wa CMG Shen Haixiong amesema mkutano wa marais wa China na Marekani uliofanyika hivi leo umefuatiliwa na dunia nzima, na mji wa San Francisco utakuwa mwanzo mpya wa uhusiano kati ya China na Marekani. Ameongeza kuwa CMG siku zote inapenda kuwa daraja la mawasiliano kati ya watu wa China na Marekani.