Wanafunzi wa sekondari wa Marekani wampa zawadi maalum rais wa China
2023-11-17 21:24:51| cri

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lincoln, Tacoma, Washington, Marekani wamempa rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan zawadi ya picha maalum waliyochora wenyewe.

Zawadi hiyo imetolewa kwenye mazungumzo ya mawasiliano ya watu kati ya China na Marekani yaliyoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Shirikisho la Mawasiliano ya Wanafunzi Vijana wa Marekani na China yamefanyika huko San Francisco, nchini Marekani.