Mkutano wa 30 wa Viongozi wa Uchumi wa APEC waanza San Francisco ukilenga mustakabali endelevu
2023-11-17 10:14:43| CRI

Mkutano wa 30 wa Viongozi wa uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) ulianza Alhamisi mjini San Francisco, Marekani, ukilenga kujenga eneo lililoungana zaidi, la uvumbuzi na jumuishi la APEC.

Akiwa mwenyekiti wa mkutano huo rais wa Marekani Joe Biden kwenye hotuba yake ya ufunguzi alisema dunia ipo katika hatua ya kubadilika ambapo maamuzi yanayofanywa sasa yataamua mwenendo wa dunia, sio tu kwa nchi chache, bali kwa matokeo ya miongo kadhaa ijayo. Amebainisha kuwa uchumi wa kila nchi unaona dalili za kile kitakachokuja kama hazitachukuliwa hatua.

Hivyo ametoa nasaha kwamba wanawajibika kwa sehemu kubwa zaidi ya kazi ya kimataifa, na ni lazima pia wawajibike kutafuta ufumbuzi wakati bado wana muda wa kubadili mwelekeo.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa, unawakutanisha viongozi wa kisiasa na kibiashara kutoka nchi 21 wanachama wa APEC.

Mkutano huo ndio lengo kuu la Wiki ya Viongozi wa APEC, inayofanyika San Francisco kuanzia Novemba 11 hadi 17, ikiwa na kaulimbiu “Kujenga Mustakabali Thabiti na Endelevu kwa Wote”.