Nchi za EA zinakubaliana juu ya mfumo wa malipo wa kikanda
2023-11-18 07:04:14| cri

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuharakisha utekelezwaji wa mfumo mmoja wa kulipia bidhaa ambapo mataifa wanachama yataweza kulipia bidhaa na huduma kwa kutumia sarafu zao. Lengo kuu la mpango huo ni kupunguza gharama na muda wa kufanya biashara kati ya mataifa husika.

Kanda na kurahisisha shughuli za kibiashara mfumo huo pia unalenga kujenga jukwaa salama za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu pamoja na mifumo ya kidijitali ya kufanya malipo. Kwa mjibu wa kamati ya kiufundi ya EAC, mfumo huu wa malipo ni miongoni mwa mipango ya kuziunganisha nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kwa njia ya kidijitali.