Rais Xi Jinping atoa wito kwa nchi wanachama wa APEC kuendelea na uvumbuzi, uwazi na kuhimiza maendeleo ya kikanda
2023-11-18 05:37:47| cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) kuendelea na uvumbuzi, uwazi, maendeleo ya kijani, na ushirikishwaji na kunufaisha pande zote katika kuhimiza maendeleo ya kikanda.

Rais Xi ameyasema hayo kwenye hotuba aliyoitoa ijumaa kwenye mkutano wa Viongozi wa Kiuchumi wa APEC mjini San Francisco, Marekani.

Rais Xi amesema China itaendelea na nia yake ya kuleta maendeleo ya amani, na kuongeza kuwa lengo la msingi la maendeleo ni kuwawezesha watu wa China kuishi maisha mazuri, si kuchukua nafasi ya mtu yeyote. Amekumbusha kuwa waka huu ni kumbukumbu ya miaka 45 tangu China ianze mageuzi na ufunguaji mlango, na kwamba China itaendelea kufuata maendeleo ya hali ya juu na yenye uwazi, na kwamba maendeleo ya China yanaweza kusaidia kuchangia kuifanya dunia kuwa ya kisasa.

Rais Xi pia ametoa wito wa kufanyika kwa juhudi za pamoja kuhimiza ushirikiano wa Asia na Pasifiki ili kupata matokeo yenye manufaa zaidi na kujenga miaka mingine 30 ushirikiano wenye manufaa wa Asia na Pasifiki.

Rais Xi pia amewaalika marafiki kutoka jumuiya za wafanyabiashara duniani kote kuwekeza na kuimarisha uwepo wao nchini China, na kusisitiza kuendelea kuwepo kwa dhamira ya China ya kutafuta maendeleo huku milango yake ikiwa wazi.

Na pia amekumbusha kuwa bila kujali jinsi hali ya kimataifa inavyobadilika, nia ya China ya kuhimiza mazingira ya biashara yenye mwelekeo wa soko, sheria na viwango vya kimataifa haitabadilika.