Mkutano wa 30 wa viongozi wa uchumi wa APEC wamalizika San Francisco
2023-11-18 15:46:40| cri

Mkutano wa 30 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC umemalizika tarehe 17 kwa saa za huko katika Kituo cha Moscone mjini San Francisco, Marekani, na kutoa "Azimio la Viongozi wa APEC mwaka wa 2023 San Francisco". Azimio hilo linasisitiza kuwa APEC inapaswa kutumia ipasavyo maendeleo ya teknolojia na uchumi ili kuendelea kuibua uwezo na uhai mkubwa wa eneo hilo, kukuza ukuaji wa uchumi, na kushughulikia changamoto zote za kimazingira, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano huo uliandaliwa na Rais Joe Biden wa Marekani, ukiwa na kaulimbiu ya "Kuunda Mustakabali Wenye Nguvu na Endelevu kwa Watu Wote."