Ziara ya rais Samia, Saudia na Morocco yavutia wawekezaji
2023-11-18 09:07:58| cri

Ziara rasmi za rais Samia Suluhu nchini Saudia Arabia na Morocco zimewavutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini humo. Mkurugenzi wa mawasiliano katika ofisi ya rais Zuhura Yunus amesema makampuni kadhaa yameonyesha nia ya kujenga viwanda nchini Tanzania siku chache baada ya rais kukamilisha ziara hizo. Kando na wawekezaji wa kigeni kuwekeza nchini Tanzania, nchini hiyo pia imepata soko jipya la bidhaa za kilimo kama nyama nchini Saudi Arabia. Hii ina maana kuwa sasa Tanzania itauza angalau tani 20, 000 za nyama nchini Saudia Arabia kila mwezi kota tani 14,000 ambazo nchini hiyo ya Afrika Mashariki huuza Saudia Arabia kila mwezi.

Kadhalika, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za Afrika zitakazofaidika kutoka na dola milioni 533 ambazo Saudia Arabia inalenga kuwekeza Afrika chini ya mpango wa Maendeleo wa Saudi Arabia SFD.