Tarehe 17 mwezi Novemba kwa saa za huko, rais Xi Jinping wa China amehudhuria Mkutano wa 30 wa Kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) uliofanyika San Francisco, Marekani.
Katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza kuwa, ni lazima kushikilia ushirikiano katika Asia na Pasifiki, changamoto zinazoikabilia dunia kwa pamoja, kutekeleza kwa pande zote Agenda ya Putrajaya, kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye ufunguaji, uchangamfu, nguvu na amani, ili kutimiza ustawi wa pamoja kwa watu wa kanda hiyo na vizazi vijavyo.