Kampuni ya sarafu ya kidijitali yashinda tuzo ya biashara bunifu Afrika.
2023-11-18 06:09:03| cri

Kampuni ya sarafu ya kidijitali yaani  Crypocurrency, kwa jina Yellow Card imeshinda tuzo ya biashara bunifu barani Afrika. Kampuni hiyo yenye makao makuu nchini Nigeria imekuwa kampuni ya kwanza ya safaru ya kidijitali barani Afrika kushinda tuzo hiyo, ishara kwamba Afrika imeanza kukumbatia sarafu za kidijitali.

 

Yellow Card ambayo sasa inatoa huduma katika nchi 20 za bara Afrika zikiwemo Rwanda, Tanzania, Burundi, Kenya na Uganda pia hutoa huduma nyingine kama vile za kufanya malipo kidijitali pamoja na kuyasaidia makampuni ya sarafu za kidijitali kuwekeza barani Afrika.