Benki ya dunia yaipongeza Tanzania kwa kusambaza maji vijijini
2023-11-18 06:34:47| cri

Makamu wa rais wa Benki ya Dunia kanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika Dkt. Victoria Kwakwa ameipongeza Tanzania kwa kuwa mfano mwema katika utekelezaji wa programu ya uendelevu wa huduma ya maji na usafi vijijini, programu ambayo inatekelezwa katika nchi 50 duniani na kufadhiliwa na benki ya dunia.

Awali, Tanzania ilipokea dola milioni 350 za Kimarekani kutekeleza mradi wa usambazaji maji kwa miaka mitano ila kwa miaka mitatu nchini hiyo ilikuwa tayari imewafikishia watu milioni 4.7 huduma za maji. Kutokana na mafanikio hayo, benki ya dunia imeongezea Tanzania dola milioni 300 kuisaidia nchi hiyo kuwafikishia watu milioni 25 huduma za maji safi.