Watu 11 wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi dogo kugonga treni jana usiku huko Lumajang, mkoani Java Mashariki nchini Indonesia.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Uokoaji wa Mkoa wa Java Mashariki, saa mbili usiku wa jana, basi dogo liligonga treni iliyokuwa ikipita katika njia ya treli isiyo na kizuizi, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu.
Polisi wamesema uchunguzi juu ya chanzo cha ajali hiyo bado unaendelea.