Rais wa sasa wa Liberia akubali kushindwa katika uchaguzi wa urais
2023-11-20 08:53:00| CRI

Matokeo ya kura zilizohesabiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Liberia yanaonyesha kuwa, makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Boakai amepata asilimia 50.64 ya kura, huku rais wa sasa George Weah akipata asilimia 49.36 ya kura.

Duru ya pili ya upigaji kura wa uchaguzi huo ilifanyika jumanne iliyopita, na ijumaa jioni, rais Weah alitangaza kupitia Kituo cha Taifa cha Radio cha Liberia kuwa, amekubali matokeo hayo, na amezungumza kwa simu na Bw. Boakai kumpongeza kwa ushindi huo.