Thamani ya makubaliano ya biashara yaliyofikiwa katika Mkutano wa CHTF 2023 yafikia dola za kimarekani bilioni 5.2
2023-11-20 08:51:23| cri


 

Mkutano wa 25 wa Kimataifa wa Biashara ya Teknolojia ya Juu wa China  (CHTF 2023) umemalizika jana, ambapo watu laki 2.48 walitembelea maonyesho hayo na thamani ya makubaliano ya biashara yalioyofikwia katika mkutano huo ikifikia dola za kimarekani bilioni 5.2.    

Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Kuhimiza nguvu ya uvumbuzi na Kuongeza sifa ya maendeleo” ulishirikisha wafanyabiashara zaidi ya 4,000 kutoka nchi na sehemu 105 duniani. Pia mkutano huo uliandaa shughuli muhimu 132, na kutangaza matokeo mapya na bidhaa mpya 681.