Kampuni ya magari ya China yapanga kujenga kiwanda cha kuunganisha magari nchini Rwanda
2023-11-20 10:58:12| cri

Kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya China Dongfeng, inapanga kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari nchini Rwanda.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uwekezaji ya Choice Africa Investments Bwana John Mugabo, ambaye ni wakala rasmi wa kampuni ya Dongfeng nchini Rwanda, amesema kama mahitaji ya magari ya kampuni hiyo yataongezeka hadi magari 200 au 300 kwa mwaka, kiwanda cha kuunganisha kitajengwa nchini Rwanda.

Kampuni ya Dongfeng inatengeneza magari ya aina mbalimbali yakiwemo malori, SUV, magari ya ujenzi, na magari ya kijeshi. Hii pia ni moja ya makampuni makubwa zaidi ya utengenezaji wa magari nchini China.