Afrika yatakiwa kuongeza uwezo wa maabara zake ili kukabiliana na vimelea sugu vya bakteria
2023-11-20 08:55:16| CRI

Nchi za Afrika zimetakuwa kukusanya fedha za ndani ili kuboresha uwezo wa maabara zao katika kupambana na vimelea sugu vya bakteria (AMR).

Akizungumza na wanahabari mjini Harare, Zimbabwe, Mratibu wa Mradi wa AMR chini ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Yewande Alimi amzitaka serikali katika nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika vifaa vya utambuzi wa vimelea sugu vya bakteria ili muundombinu sahihi uweze kutumika.

Naye mtaalamu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Walter Fuller amesema, mtazamo wa uratibu unatakiwa kati ya nchi za Afrika ili kukabiliana na vimelea sugu wa bakteria. Amesema tafiti za karibuni zinaonyesha kuongezeka kwa athari za kiuchumi na kijamii kutokana na vimelea sugu hivyo, na kwamba huu ni muda sahihi kwa nchi za Afrika kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo hilo.