Serikali ya Tanzania kuendelea kuongeza watumiaji huduma za kifedha
2023-11-20 10:59:22| cri

Serikali imepanga hadi ifikapo mwaka 2025, asilimia 80 ya Watanzania wawe wamefikiwa na huduma za kifedha ikiwemo benki, masoko ya dhamana za mitaji, huduma za bima, huduma za mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Ili kufikia idadi hiyo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha, inajitahidi kuhakikisha kuwa watu wawe wamefikiwa na huduma hizo kwa kutoa elimu ya umuhimu wa matumizi ya huduma hizo.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Idara ya uendelezaji sekta ya Fedha, Dk Charles Mwamwaja, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya wiki ya taifa ya huduma za fedha inayofanyika mjini Arusha.