Watu zaidi ya 13,000 wauawa katika mashambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza
2023-11-20 08:52:11| cri

Kundi la Hamas la Palestina jana limesema, mashambulio ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 13 na kujeruhi zaidi ya watu elfu 30 tangu mapigano mapya kati ya Palestina na Israel yalipozuka.

Katika taarifa yake, kundi hilo limesema zaidi ya watoto 5,500 na wanawake zaidi ya 3,500 ni miongoni mwa watu waliofariki, na takriban watu 6,000 hawajulikani walipo. Mapigano hayo pia yamesababisha vifo vya wafanyakazi wa afya 201, walinzi 22 wa raia na waandishi wa habari 60. Pia, hospitali 25 na vituo vya afya 52 katika Ukanda wa Gaza vimefungwa.