Karakana ya Luban ya China yafungua shule ya ufundi nchini Rwanda
2023-11-20 08:54:43| CRI

Karakana ya Luban inayoungwa mkono na Chuo cha Ufundi Stadi cha China imefunguliwa nchini Rwanda kupitia ushirikiano na Chuo cha Ufundi Anuai cha Rwanda na Chuo cha Ufundi Anuai cha Jinhua cha mkoani Zhejiang, mashariki mwa China.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Kaimu mkuu wa Chuo cha Ufundi Anuai cha Rwanda, Sylvie Mucyo amesema, karakana hiyo imeanzishwa na teknolojia za kisasa ambazo zinahitajika katika dunia ya sasa. Ameongeza kuwa, hatua hiyo ni mafanikio makubwa kwa kuwa itawasaidia wanafunzi wa Rwanda kupata elimu bora na mafunzo bora katika mazingira mazuri.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Rwanda Wang Xuekun amesema, kwa juhudi za pamoja za Chuo cha Ufundi Anuai cha Jinhua na kile cha Rwanda, IPRC Musanze kimekuza vipaji vya vijana wengi nchini Rwanda. Amesema kuna haja ya kuweka mazingira wezeshi kwa karakana hiyo kufaidisha vijana wengi zaidi nchini Rwanda.