Waziri Mkuu wa China atuma salamu za pongezi kwa Waziri Mkuu mpya wa Algeria
2023-11-21 09:52:28| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang jana amempongeza Bw. Ennadir Larbaoui kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Algeria.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya simu, Bw. Li amesema, serikali ya China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili. Amesema anapenda kushirikiana na Bw. Larbaoui kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuendelea kuimarisha uaminifu wa kisiasa, kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, na kuhimiza maendeleo zaidi ya ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa China na Algeria.