Kikosi cha RSF cha Sudan chatangaza kudhibiti eneo la kusini mwa Khartoum
2023-11-21 23:09:41| cri

Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF) kimetoa taarifa kikitangaza udhibiti kamili wa eneo la Jabal Oliya kusini mwa mji mkuu Khartoum, ikiwa ni pamoja na kambi ya jeshi la anga katika eneo hilo na Daraja la bwana la Jabal Oliya.  

Eneo la Jabal Oliya liko takriban kilomita 40 kusini mwa Khartoum na ni moja ya njia kuu katika mzunguko wa mji mkuu kutoka magharibi mwa Sudan. Jeshi la Sudan (SAF) lina kambi ya jeshi la anga katika eneo hilo na vikosi kadhaa vya helikopta. Hivi karibuni, vikosi cha RSF na jeshi la Sudan vilipambana vikali kugombea kambi hii na Daraja la Jabal Oliya. RSF walitoa taarifa ya kutwaa udhibiti wa kituo hicho.