Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza
2023-11-21 08:44:36| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea tena wito wake wa kutaka kusitisha vita kwa sababu za kibinadamu, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya vifo katika Ukanda wa Gaza.

Amesema vita hiyo imesababisha vifo vya idadi kubwa ya watu, wakiwemo wanawake na watoto kila siku, na amerejea tena wito wake wa kusimamisha vita hiyo kwa sababu za kibinadamu.

Bw. Guterres amesema maelfu ya Wapalestina wanatafuta hifadhi katika maeneo ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Gaza kutokana na kuongezeka kwa mapigano.