Marais wa China na Ufaransa wazungumza kwa simu
2023-11-21 08:43:06| CRI

Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu amezungumza kwa simu na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Rais Xi amesema, mwaka 2024 utakuwa maadhimisho ya miaka ya 60 tangu kuanzisha kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Ufaransa. Amesema China inapenda kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na Ufaransa, kuhimiza kupata maendeleo mapya katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za elimu, utamaduni na utafiti wa sayansi, na kuhimiza mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake rais Macron amesema, kutokana na hali ya sasa ya dunia, kudumisha mawasiliano na ushirikiano wa kimkakati kwa pande hizo mbili kutakuwa na umuhimu mkubwa. Ameongeza kuwa, Ufaransa inapenda kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yake na China, kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu, na kukuza mawasiliano na ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara, usafiri wa anga na utamaduni.

Viongozi hao wawili pia walibadilishana maoni kuhusu mgogoro kati ya Palestina na Israel, na kusema kipaumbele kwa sasa ni kuepuka hali ya Palestina na Israel kuwa mbaya zaidi, na kwamba “Mpango wa Nchi Mbili” ni njia ya kimsingi ya ufumbuzi wa mgogoro huo.