Kazi ya uwekaji wa mitambo ya juu ya ardhi ya bomba la mafuta kutoka Uganda-Tanzania inafanyika
2023-11-21 14:16:45| cri

Mkandarasi mkuu wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki lenye urefu wa maili 900 (EACOP) kutoka Hoima magharibi mwa Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania, ameanza kazi za kuwekewa mitambo ya juu ya ardhi katika nchi zote mbili. Haya yanajiri wakati mradi huo unaingia katika kipindi muhimu cha miezi 24 cha mwisho cha ujenzi wa bomba hilo, unaotarajiwa kugharimu dola bilioni 5.

Wiki iliyopita kampuni ya Pearl Engineering Ltd, mkandarasi mdogo wa kazi za utayarishaji wa eneo la kazi ilikabidhi moja ya maeneo yatakayokuwa yadi ya bomba kuu la kambi na kituo cha pampu moja katika Wilaya ya Hoima, Uganda, kwa mkandarasi mkuu wa ujenzi wa bomba, yaani kampuni ya CPP ya China.

Wiki hii CPP ilianza kazi ya ujenzi wa kituo cha kwanza kati ya vituo viwili vya pampu vya Eacop nchini Uganda, wakati vingine vinne viko Tanzania, ambavyo kila kimoja kitakuwa na tani 40 za kusukuma na kudumisha mtiririko wa mafuta ghafi ya Uganda.