Boakai atangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Liberia
2023-11-21 09:08:25| cri


 

Tume ya Uchaguzi ya Liberia imemtangaza Joseph Boakai kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais na kumshinda rais wa sasa wa nchi hiyo, George Weah.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Davidetta Browne Lansanah amewaambia waandishi wa habari jana baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu kura, Boakai alipata asilimia 50.64 ya kura, na Weah alipata asilimia 49.36 ya kura.