Serikali ya Sudan Kusini na chama cha upinzani cha Sudan vyatoa wito wa kusimamisha mapigano
2023-11-22 08:39:38| CRI

Serikali ya Sudan Kusini imekutana na wajumbe wa muungano wa vyama vya kiraia vya Sudan, Harakati za Uhuru na Mabadiliko (FFC) jana jumanne, ikiwa ni katika juhudi za kusimamisha mapigano kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kisiasa yanayolenga kumaliza mapigano yaliyoanza April 15 mwaka huu nchini Sudan.

Kiongozi wa FFC Omar El Degeir amesisitiza haja ya pande za kisiasa za nchini Sudan kukubaliana kuhusu utawala wa kidemokrasia, muungano wa jeshi, na ufufukaji wa uchumi kupitia majadiliano.

Katibu mkuu wa tume ya upatanishi ya Sudan Kusini, Dhieu Mathok Diing Wol amesema, rais wa nchi hiyo Salva Kiir ameratibu mikutano na mashauriano na mashirika ya kisiasa na kiraia ya Sudan kuhusu mapigano hayo.